![]() |
|||||
| Iwapo MOJA kati ya taarifa nne hapo juu siyo sahihi na hailingani na mamalia unayemchunguza, usichague 1A), (hata kama taarifa zingine zote ni sahihi). 3) Inabidi kuangalia kwa makini KILA neno lililopo kwenye taarifa: Kucha bapa za miguu ya nyuma ina maana MIGUU YA NYUMA, siyo ya mbele; Kuna meno kwenye taya ya juu NA kuna meno kwenye taya ya chini ni tofauti na Kuna meno kwenye taya ya juu AU kuna meno kwenye taya ya chini.
5) Utakapofika mwisho wa zoezi na kuona picha hazifanani na kielelezo unachochunguza, rudia tena zoezi toka mwanzo (HOME-KEY) na fuata maelekezo yote kwa uangalifu. Inawezekana kabisa kwamba baadhi ya taarifa zimeorodheshwa zaidi ya mara moja. 6) Nchini Tanzania, kama ilivyo katika nchi nyingine, spishi zinagunduliwa kwenye maeneo mapya. Spishi mpya katika sayansi pia zinazidi kugunduliwa. Inawezekana kwamba spishi unayochunguza haijawahi kugunduliwa Tanzania na kwa hiyo haiko kwenye orodha yetu hii. 7) Wakati mwingine, utalazimika kuhesabu meno ya pande zote mbili za taya moja. Kwa tahadhari, hesabu meno ya pande zote mbili hizo. Iwapo idadi inatofautiana kati ya pande mbili, chukua idadi ya juu zaidi. 8) Kwa sasa, taarifa zinakomea kwenye kiwango cha jenasi, ingawa kwa baadhi ya jenasi kuna spishi moja tu, kwa mfano muhanga na kifaru. Iwapo kuna zaidi ya spishi moja kwenye jenasi, spishi zingine zitaongezwa baadaye, ili kumwezesha mtumiaji abainishe spishi ya kielelezo anachochunguza. 9) Baadhi ya sifa (features) zinapatikana kwenye jenasi zaidi ya moja (hasa kuhusu ngozi). Kuna mashaka juu ya uhalali wa baadhi ya jenasi hizi: kwa hiyo kuna haja ya kufanya utafiti zaidi ili kuweza kubainisha jenasi mbalimbali za mamalia. 10) Kazi ya kutafsiri "SIFA NA TAARIFA ZA MAMALIA WA TANZANIA" imetoa changamoto. Changamoto kubwa ilikuwa kutafuta namna inayokubalika ya kuelezea ujumbe, kwa sababu Kiswahili bado kina upungufu wa maneno katika nyanja inayohusika. Kwa hiyo maneno mengi ya Kiingereza na Kilatini yametumika katika tafsiri hii. Inawezekana kabisa kwamba hili ni jaribio la kwanza la kutumia Kiswahili ili kuweka taarifa za namna hii kwenye webu. Kwa hiyo tungependa wasomaji waichukulie tafsiri hii kama hatua ya mwanzo katika kutafuta tafsiri bora zaidi, kazi ambayo itategemea sana mchango wa wasomaji. Wasomaji wanaombwa kuwasilisha maoni iwapo kuna mambo ambayo siyo sahihi, maana haileweki, au wangependa kuboresha tafsiri hii kwa namna moja au nyingine. Tunatumaini kwamba taarifa hizi zitakuwa na manufaa kwenu na tunawatakia heri! |
|||||
Kiswahili Home | Maelekezo | Fuu | Ngozi | Safu Za Milima Ya Mashariki | Zoology | Field Museum Home | Shukrani Na Marejo | Tanzanian Mammal Key (English Version) © 2001 The Field Museum, All Rights Reserved 1400 S. Lake Shore Dr., Chicago, IL 60605-2496 312.922.9410 |
|||||