Safu za Milima ya Mashariki ni mlolongo wa safu zilizotengana za milima yenye vilele; vilele hivi vinaonekana kama mwezi mwandamo (crescent pattern) na safu hzi zinapatikana mashariki mwa Tanzania. Milima hii iliundwa mamilioni ya miaka iliyopita, na ina spishi nyingi kuliko eneo lingine lolote la milima barani Afrika; baadhi ya spishi hizi ninapatikana katika eneo hili tu. Kutokana na utajiri huu wa spishi, milima hii imepewa jina la “Visiwa vya Galapagos vya Afrika”. Ingawa wanasayansi wanajua kuwa milima hii ina spishi za pekee, kuna taarifa chache sana juu ya biolojia ya viumbe vinavyoishi katika miinuko ya juu sana. Hali inasikitisha, kwani mazingira katika misitu hii yanabadilika na kuharibiwa kwa kasi kubwa.

Kwa kipindi cha miaka kumi sasa, wataalam kutoka The Field Museum na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wanafanya utafiti juu ya ikolojia na maeneo ya mamalia wadogo wa Safu za Milima ya Mashariki. Mpaka sasa, tumetembelea baadhi ya safu kubwa za milima na kukusanya taarifa juu ya “shrews”, popo na “rodents” wanaoishi katika misitu ya milima hii. Kutokana na kazi hii na pia kutokana na tafiti zingine zilizokusanya vielelezo vya wanyama, spishi mpya kadhaa za mamalia zimegunduliwa na ufahamu wetu juu ya biolojia ya mamalia hawa umeongezeka. “Shrew” ndio wenye spishi nyingi zinazopatikana katika eneo hili peke yake, wakifuatiwa na “rodents”. Spishi kadhaa za “rodents” zinapatikana katika sehemu kubwa ya Safu za Milima ya Mashariki lakini hazipatikani katika sehemu za chini ya milima hii. Mamalia wadogo kutoka kila safu ya milima hii zinatuonyesha kwamba Safu za Milima ya Mashariki hazina kifani; aidha mamalia hawa wanaweza kutusaidia kuona jinsi ambavyo tunaweza kuhifadhi aina hii ya pekee ya milima.



Kiswahili Home | Maelekezo | Fuu | Ngozi | Safu Za Milima Ya Mashariki | Zoology |
Field Museum Home | Shukrani Na Marejo | Tanzanian Mammal Key (English Version)

© 2001 The Field Museum, All Rights Reserved
1400 S. Lake Shore Dr., Chicago, IL 60605-2496
312.922.9410