“Shrews” ni wanyama wanaopatikana kwa wingi katika misitu ya Safu za Milima ya Mashariki. Kuna pengo kubwa kuhusu taarifa za kibiolojia (natural history) juu ya aina hii ya wanyama na juu ya mahusiano na mabadiliko (evolutionary relationships) baina ya spishi tofauti. Utafiti juu ya wanyama hawa utatupatia taarifa zaidi juu ya historia ya mamalia wa Safu za Milima ya Mashariki na juu ya ekolojia ya misitu ya milimani.

Crocidura – Musk shrews

Inakisiwa kwamba kuna spishi 23 za Crocidura nchini Tanzania. Idadi hii itabadilika kadri utafiti unapofanywa na kugundua spishi zingine. Baadhi ya wanyama wanaoishi kwa wingi katika misitu ya Safu za Milima ya Mashariki ni: C. olivieri (Crocidura mkubwa kuliko wote Tanzania), C. monax, C. hildegardeae na C. elgonius (mmoja wa “musk shrews” wadogo kabisa Tanzania). Crocidura desperata anapatikana Udzungwa tu na yuko hatarini kutoweka.




Myosorex – Mouse-shrews

“Mouse shrew” ana mkia mfupi na miguu yenye magamba mengi. Spishi mbili zinapatikana Tanzania: M. geata na M. kihaulei. Spishi ya M. kihaulei ilipewa jina hilo karibuni baada ya kukusanya vielelezo kutoka milima ya Udzungwa; vielelezo hivyo vilionyesha kwamba M. kihaulei ina maumbile madogo ya fuu ukilinganisha na M.geata (inayopatikana milima ya Uluguru). Myosorex inapatikana pia kwenye Mlima Rungwe.


Sylvisorex – “Shrew” wa Msituni

Spishi nne zinapatikana Tanzania. Mbili kati ya hizo zinapatikana kwa wingi katika misitu ya Safu za Milima ya Mashariki: S. megalura na S. howelli. S. megalura ina mkia mrefu sawa na kichwa na mwili kwa pamoja, na pengine ni mrefu zaidi. S. howelli inapatikana katika misitu ya Safu za Milima ya Mashariki tu. Ingawa S. howelli ni wengi katika milima wanakopatikana, wao wanaonekana tu katika maeneo yafuatayo ya misitu ya Safu za Milima ya Mashariki: Usambara ya Mashariki, Usambara ya Magharibi, Uluguru, Nguru, Ukaguru and Milima ya Nguu.


Suncus – “Shrew” kibushuti

Ingawa Suncus murinus ni mmoja wa “shrews” wakubwa Tanzania (inaelekea sio mwenyeji wa hapa, ila aliletwa kutoka nje), spishi mbili nyingine zinazopatikana nchini (S. lixus na S. varilla) ni ndogo. Kwa kawaida, S. lixus haipatikani kwa wingi katika misitu ya Safu za Milima ya Mashariki; hata hivyo spishi hii imeonekana katika misitu yenye mvua kidogo ya Milima ya Udzungwa.



Kiswahili Home | Maelekezo | Fuu | Ngozi | Safu Za Milima Ya Mashariki | Zoology |
Field Museum Home | Shukrani Na Marejo | Tanzanian Mammal Key (English Version)

© 2001 The Field Museum, All Rights Reserved
1400 S. Lake Shore Dr., Chicago, IL 60605-2496
312.922.9410