Watu wamezoea sana kuona “rodents” kwa sababu wanaishi kwenye makazi ya binadamu. Lakini “rodents” wanaoishi kwenye misitu ya Safu za Milima ya Mashariki ni tofauti. Kuna aina maalum ya panya (mice and rats) wanaoishi katika sehemu kubwa au katika eneo lote la misitu ya Safu za Milima ya Mashariki; aina hii hupatikana tu katika miinuko ya juu sana ya milima. Kinyume na “shrews” wa Safu za Milima ya Mashariki, inaelekea hakuna aina maalum ya “rodents” wanaoishi katika maeneo maalum ya Safu za Milima ya Mashariki.

Praomys delectorum
Panya mwenye manyoya laini wa Afrika ya Mashariki

Praomys ni aina ya “rodents” inayopatikana kwa wingi sana katika misitu ya Safu za Milima ya Mashariki; ana manyoya laini ya kahawia, mkia mrefu na sehemu ya chini ya tumbo lake ni jeupe na chafu. Mara nyingi watu wanamchanganya na Hylomyscus, lakini Praomys ana pua ndefu zaidi na kwato nyeusi (dark soles) za miguu ya nyuma (ambayo ni mirefu zaidi pia); hana manyoya mwishoni mwa mkia.

Praomys delectorum anaishi zaidi juu ya ardhi na hupatikana chini ya ardhi kwa nadra katika misitu ya Safu za Milima ya Mashariki. “Rodents” hawa wanakula mbegu, majani (vegetation) na wadudu.


Hylomyscus denniae -
Panya wa Misitu ya Milima ya Afrika ya Mashariki

Ingawa Hylomyscus sio wengi kama Praomys, wanapatikana mara nyingi katika misitu ya Safu za Milima ya Mashariki. Mara nyingi, watu wanamchanganya Hylomyscus na Praomys, lakini Hylomyscus ana pua fupi zaidi, kwato zilizopauka za miguu ya nyuma (ambayo ni mifupi zaidi) na hana manyoya mwishoni mwa mkia.

Panya huyu anaishi chini ya ardhi na anakula mimea inayokwea, matawi na hata matawi madogo kabisa ya miti na vichaka. Chakula chake kinafanana na cha Praomys.


Grammomys -
Panya wa Vichakani

“Rodents” hawa wazuri wana mikia mirefu yenye manyoya, tumbo jeupe kabisa na manyoya ya mgongoni yenye rangi ya chungwa au nyekundu hafifu. Grammomys sio wengi kama Praomys au Hylomyscus katika eneo la misitu ya Safu za Milima ya Mashariki. Ingawa spishi hii haijatambuliwa kikamilifu katika jenasi yake, inasadikiwa kwamba spishi tatu zinapatikana kwenye misitu ya Safu za Milima ya Mashariki, nazo ni Grammomys dolichurus, Grammomys ibeanus, na Grammomys macmillani.

Panya wa Vichaka ni wakweaji wazuri na wanakula majani (vegetarian) kwa ujumla lakini wanakula wadudu pia.


Lophuromys flavopunctatus
Panya wa Vichakani mwenye manyoya

Lophuromys ni panya aliye tofauti kabisa, mwenye manyoya ya mgongoni mekundu sana na tumbo lenye rangi ya machungwa. Manyoya yake ni magumu, sio laini na mkia wake mara nyingi unakatika na kubakia kipande kifupi tu. Lophuromys ni aina ya “rodent” inayopatikana kwa wingi zaidi kwenye misitu mingi ya Safu za Milima ya Mashariki.

TChakula chao hasa ni wadudu, lakini panya hawa wanakula pia wanyama wengine wenye uti wa mgongo (vertebrates), “carion” na mimea. “Rodents” hawa wanaishi juu ya nchi tu.


Beamys hindei – Lesser Pouched Rat

Beamys ana manyoya ya kijivu, tumbo jeupe na mkia wenye rangi zilizofifia na ambao ni mweupe mwishoni. “Rodent” huyu ana uhusiano na Cricetomys. Inaelekea kwamba spishi mbili za Beamys zinapatikana katika Safu za Milima ya Mashariki: Beamys hindei na Beamys major. Inabidi kufanya utafiti zaidi juu ya “rodent” huyu.

“Rodents” hawa ni wakweaji wazuri na wanakula mbegu na matunda na hubeba vyakula hivi kwenye mifuko yao ya mashavuni.



Kiswahili Home | Instructions | Fuu | Ngozi | Safu Za Milima Ya Mashariki
Zoology | Field Museum Home | Credits | Tanzanian Mammal Key (English Version)


© 2001 The Field Museum, All Rights Reserved
1400 S. Lake Shore Dr., Chicago, IL 60605-2496
312.922.9410